Mbunge wa jimbo la kilwa kusini Seleman Bungara akiongea na
wananchi wa Nangurukuru kilwa ambapo alishukuru Uwepo wa gesi asilia Kunavyochangia maendeleo ya Kilwa
Na Abdulaziz Ahmeid,Kilwa Masoko
Mbunge wa jimbo la Kilwa kusini Saidi Bungara (CUF) amelaani kitendo cha baadhi ya wananchi mikoa ya Lindi na Mtwara kukwamisha juhudi za serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi kupitia uwekezaji wa gas ya asili nchini.
Haya ameyaeleza kwenye hafla fupi ya kutiliana sahini mkataba wa
ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Nangurukuru kati ya halmashauri ya
wilaya Kilwa na kampuni ya Afrikan Energy Inayojihusisha na utafiti
wa mafuta na gesi.
Bungara alisema kitendo cha mwekezaji huyo kuwafanyia maendeleo
wananchi wa wilaya hiyo ni ishara tosha ya kutambua michango na
juhudi za wawekezaji katika kutoa huduma za kijamii kwa wananchi.
‘Kitendo cha mwekezaji wa pan African Energy kutoa misaada yenye lengo la kuboresha huduma za kijamii zimethihirisha ukweli wa serikali kuhusu faida na maana ya wawekezaji, sisiwa Kilwa hatuwaungi mkono wa Mtwara tuna sema itoke tu” alisema Mbunge Bungara
Alisema watu wa kilwa hawana sababu kupinga ya kupinga uwekezaji wa namna yoyote kwani wanachohitaji ni maendeleo na sio vurugu na fujo kama wanavyofanya wananchi wa mkoa wa mtwara kupinga kuondoka kwa kesi .
Kwa upande wake Meneja wa huduma za jamii wa kampuni ya Pan Afrikani Energy Andrew Kashangaki alisema kampuni inafadhiri ujenzi wa zahanati ya Nangurukuru na unatarajia kutumia zaidi ya shs milioni
234,714,980, Kashangaki alisema sambamba na kusaidia ujenzi wa zahanati hiyo pia kampuni hiyo inalipa ushuru wa huduma ambapo hadi sasa imelipa kwa halmashauri hiyo zaidi ya shs milioni 638 na inatoa misaada mingine katika sekta ya elimu.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.