MATUMAINI AANZA KUJIKONGOJA

clip_image001

Na Gladness Mallya
BAADA ya kutoka nchini Msumbiji akiwa hoi, msanii wa vichekesho Bongo, Tumaini Mwakibibi ‘Matumaini’ hatimaye amepata nguvu na ameanza kujikongoja katika kazi ya uigizaji.

Akichonga na paparazi wetu hivi karibuni, Matumaini alisema kwa sasa anaendelea vizuri na ameshaanza kucheza filamu mbalimbali anazoshirikishwa na wasanii wenzake na sasa anaendesha maisha yake mwenyewe.

“Nawashukuru sana wasanii wenzangu kwani kama siyo wao, ningerudishwa nikiwa maiti, sina cha kuwalipa ila Mungu ndiye atakayewalipa,” alisema Matumaini.

Hata hivyo, alilaani vikali baadhi ya wasanii wanaozusha maneno ya uongo kwamba Michael Sangu alikula fedha alizokuwa anachangisha kwa ajili yake jambo ambalo siyo la kweli.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post