Baadhi ya Wakazi wa Mji wa Mtwara na vitongoji vyake wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri kwenye semina ya Fursa kwa Vijana iliyofanyika mapema leo ndani ya ukumbi wa Pentecoste Ligula B,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana mkoani Mtwara.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba (ambaye pia ni mzaliwa wa Newala mkaoni Mtwara),Mh.Yahya Nawanda akizungumza na wakazi wa mji wa Mtwara waliojitokeza kwa wingi kwenye semina ya Fursa kwa Vijana mapema leo,Mh.Yahya alizunguma mengi zikiwemo fursa mbalimbali zinazopatikana ndani ya mkoa wa Mtwara na Singida namna ya kuzifanyia kazi katika suala zima la kujikwamua na maisha.
Mkurugenzi wa Vipindi Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akihitimisha semina ya Fursa kwa Vijana mapema leo mchana,ndani ya ukumbi wa ukumbi wa Pentecoste Ligula B,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana Mtwara,kulia kwake ni Meneja Kiongozi,Uhusiano NSSF Makao makuu jijini Dar,Eunice Chiume pamoja na Meneja wa NSSF mkoani Mtwara Bwa.Stanley Mullanzi.Semina ya Fursa kwa vijana tayari imekwishafanyika mikoa ya Tabora,Kigoma,Singida na sasa Mtwara.
Tags
HABARI ZA KITAIFA