ARSENAL YAKARIBIA KUMNASA KIUNGO WA BAYERN MUNICH

clip_image001Arsenal inakaribia kukamilisha usajili wa kiungo wa kimataifa wa Brazil Luis Gustavo toka klabu ya Bayern Munich .

Arsenal na Munich zimefikia makubaliano juu ya bei ya kiungo huyo ambayo itakuwa euro milioni 20 kabla ya kufanya mazungumzo na mchezaji mwenyewe .

Gustavo aliambiwa wazi na kocha wa Bayern Pep Guardiola kuwa hataweza kupata nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza hali inayomfanya atafute timu ya kwenda ambayo itamhakikishia nafasi kwenye kikosi chake .

clip_image001[5]Endapo usajili huu utakamilika utakuwa na ahueni kubwa kwa mashabiki wa Arsenal ambao wamekuwa kwenye huzuni baada ya kumkosa mshambuliaji Gonzalo Higuain ambaye kwa muda mrefu alidhaniwa kuwa mbioni kujiunga na Arsenal kabla ya kujiunga na Napoli .

Pamoja na Higuain Arsenal imeshuhudia ofa zake mbili za kumsajili mshambuliaji Luis Suarez zikikataliwa na Liverpool ambayo imeshikilia uamuzi wa kutomuuza mshambuliaji huyo .

Hadi sasa Arsenal imesajili mchezaji mmoja pekee ambaye ni mchezaji wa timu ya vijana ya Ufaransa Yaya Sanogo.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post