Tupeni jamani tupeni!: Arsenal wamejiandaa kutuma ofa nyingine ya pauni milioni 35 wiki hii kwa majogoo wa jiji, Liverpool ili kumsajili Luis Suarez
Washika bunduki wa kaskazini mwa London nchini England, klabu ya Arsenal wamejipanga tena kutuma ofa ya pauni milioni 35 wiki hii ili kuinasa saini ya mshambuliaji wa majogoo wa jiji ama Wekundu wa Anfield, klabu ya Liverpool, raia wa Uruguay, Luis Suarez.
Suarez amekuwa chagua namba moja kwa kocha wa Arsenal majira haya ya kiangazi ya usajili barani Ulaya, Mfaransa, Arsene Wenger na sasa anaandaa kitita hicho ingawa Liverpool walisema kama anataka kumsajili nyoya huyo anatakiwa kulipa ada ya uhamisho ya pauni milioni 40.
Awali Wenger alituma ofa ya pauni milioni 30 na Liverpool wakataa, sasa wiki hii ameongeza pauni milioni 5 na kufikia 35, lakini sijui kama Liver watakubali kwani walishasema wanahitaji 40 na si vinginevyo.
Mshabiki wa Arsenal wana imani kubwa kuwa mshambuliaji huyo mwenye matatizo makubwa nchini England ataweza kuwasili Emirates, na wanataka kitita cha pauni milioni 70 alichopewa Wenger kwa ajili ya usajili kitumike kumleta kaskazini mwa London.
Wenger yupo katika presha kubwa ya kusajili wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu kutokana na klabu hiyo kusema kuwa kwa sasa ina uwezo wa kushindana katika soko la kutafuta wachezaji ghali zaidi duniani.
Liverpool wanahitaji mzigo wa pauni milioni 40 ili kumuachia Suarez, huku Arsenal wakigongwa vichwa vibaya sa
Karudi kibaruani: Brendan Rodgers pamoja na kikosi chake cha Liverpool amerudi kupiga kazi kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu England
Namhitaji jamani, kubalini tu!: Bosi wa The Gunners , Arsene Wenger yupo tayari kuvunja benki majira haya ya kiangazi ili kumsajili Suarez
Wasiwasi mkubwa: Dili la Gonzalo Higuain huenda limeshindikana baada ya Wenger kuelekeza nguvu zake kwa Suarez