WANAMGAMBO 3 WA AL-SHABAAB WAUAWA KWENYE MLIPUKO MOGADISHU

clip_image001Watu watatu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa al-Shabaab walikufa baada ya kifaa cha mlipuko walichokuwa wakikitega kulipuka kwenye wilaya ya Wadajir, Mogadishu, siku ya Jumanne asubuhi (tarehe 23 Julai), iliripoti Redio Bar-Kulan inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa.

Mlipuko huo ulilitikisa jengo la karibu na mwanamke mmoja alijeruhiwa, ingawa haikuwa wazi ikiwa alikuwamo ndani ya jengo hilo wakati bomu lilipolipuka.

Vikosi vya usalama vya Somalia vililifunga haraka eneo hiyo na kuanza upelelezi.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post