Kipaji cha muziki cha Vanessa Mdee kilianza kujulikana baada ya sauti yake kusikika kwenye wimbo wa AY ‘Money’ na kisha kukidhihirisha zaidi kwenye ‘Me and You’ alioshirikishwa na Ommy Dimpoz. Mwanzo mwa mwaka huu alipotoa single yake ya kwanza, ‘Closer’ ndipo watu wakashtuka kwamba kumbe mtangazaji huyu wa MTV Base na Choice FM ana kipaji cha kuimba.
Kuanzia hapo Vanessa Mdee ameshafanikiwa kupanda kwenye stage mbalimbali kubwa kuperform na wasanii wakongwe wa nchini. Lakini kwanini alichelewa sana kuingia kwenye muziki? Vanessa amefunguka kwenye show ya Mkasi kuwa mwanzoni alikuwa hajiamini.
“Music is my first love kwakweli kusema ukweli ningependa nianze kama mwanamuziki, lakini nilikuwa bado sina ile confidence, nilikuwa bado sijakamilika, unajua mimi naamini kwamba kama hauko ready kufanya kitu fulani, Mungu hawezi kukutayarishia hivyo vitu. When I started working for MTV nilikuwa mdogo, I was 19, nilikuwa chuo, bado nilikuwa namtegemea mama kwa kiasi fulani, so I think ukimwambia mzazi kwamba unataka kufanya muziki, anakuambia ‘are you mad’.
So for years nilikuwa najitrain na if you ask anyone ambaye nimekua naye zamani nilikuwa nafanya muziki sana, high school nilikuwa naimbiaga watu kwenye bweni, chombeza time tulikuwa tunaita,” alisema Vanessa.
CHEKI SHOW HAPO CHINI