JOSE MOURINHO amesisitiza kwamba sasa ni uamuzi wa mwisho kuhusu usajili wa Wayne Rooney umebaki mikononi mwa klabu ya Manchester United.
Chelsea leo mchana ilithibitisha kwamba wametuma ofa rasmi ya kumsajili Rooney lakini United wameikataa
Lakini muda mfupi uliopita Mourinho amethibitisha kwamba Rooney ndio mchezaji pekee anayemhitaji kwenye kikosi chake.
"Nadhani kila kitu kipo wazi sasa - sio siri tena. Ofa rasmi imetumwa lakini ilikuwa ya kiasi cha fedha na haikuhusisha mchezaji yoyote. Tunamhitaji mchezaji. Tumetuma ofa na sasa hatuna cha kusema zaidi. Tumewaachia Manchester United waamue.”
Tags
SPORTS NEWS