CHELSEA WAIPA UNITED JUAN MATA AU DAVID LUIZ NA PAUNDI MILIONI 10 JUU WAPEWE ROONEY...LAKINI MASHETANI WEKUNDU WATOA NJE KIKUDA

ManchesterUnitedAirbus2KLABU ya Manchester United imekataa ofa ya kwanza ya Chelsea kwa ajili ya Wayne Rooney - Pauni Milioni pamoja na mchezaji.
FAHARI YA KUSINI inafahamu wachezaji wawili walioambatanishwa katika ofa hiyo United ichagua mmoja ni Mchezaji Bora wa Mwaka, Juan Mata au beki Mbrazil, David Luiz.
United imesema Rooney hauzwi na kocha wa Chelsea, Jose Mourinho sasa lazima aamue kuweka gungu tu la maana la fedha mezani.Something on your mind? Wayne Rooney arrives at Manchester United's training ground on WednesdayLolote mawazoni mwako? Wayne Rooney akiwasili viwanja vya mazoezi vya Manchester United leo kwa mazoezi
Arsenal pia imetoa ofa ya awali ingawa pia imetoa ofa kwa Luis Suarez na Gonzalo Higuain.Klabu hiyo ya Stamford Bridge imeonywa, isithubutu kurejea na ofa ya pili, kwani United haina mpango wa kumuuza Rooney kwa klabu nyingine ya Ligi Kuu England.
Mourinho yu tayari kuwauza Mata na Luiz, ili fedha atakazopata kutokana na mauzo ya wawili hayo atumie kumnunua mchezaji wa United.
Rooney anafikiri amefikia kilele cha mustakabali wake na hana zaidi cha kuthibitisha baada ya misimu tisa Old Trafford.
Inafahamika mshambuliaji huyo wa England amechanganyikiwa na kukerwa na maneno ya kocha mpya, David Moyes kwamba hatauzwa sababu ndiye mbadala wa mshambuliaji chaguo la kwanza, Robin van Persie.Up for grabs? Chelsea have offered Juan Mata (above) or David Luiz (below) in part-exchange for RooneyChelsea imewaofa United Juan Mata (juu) au David Luiz (chini) pamoja na Pauni Milioni 10 wapewe RooneyDavid LuizMourinho aliwasha moto jana katika jitihada zake za kuwania saini ya Rooney kwa kutoa onyo kwamba, matumaini ya England yatakuwa madogo Kombe la Dunia kama mchezaji huyo atabakia United.
Chelsea imehamishia nguvu zake kwa Rooney baada ya wachezaji iliyokuwa inawataka awali kuwakosa wote, Radamel Falcao amekwenda Monaco na Edinson Cavani katua PSG, zote za Ufaransa.
Mourinho alisema: "Ikiwa Wayne ni chaguo la pili kwa Manchester United, kisha timu ya taifa itaathirika.’
HII NDIYO SABABU CHELSEA INAWATOA JUAN MATA AU DAVID LUIZ?MATA LUIZ
Umri: Miaka 25
Nafasi: Kiungo mshambuliaji
Klabu za awali: Real Madrid B, Valencia
Takwimu za Chelsea: 2011-12: Mechi: 54 Mabao: 12
Pasi za mabao: 23
2012-13: Mechi 64 Mabao 20 Pasi za mabao 35
Hispania: Mechi: 29 Mabao 8.





Umri: Miaka 26
Nafasi: Beki/Kiungo
Klabu za awali: Vitoria, Benfica
Takwimu za Chelsea: 2010-11: Mechi:12 Mabao: 2
2011-12: Mechi 40 Mabao 3
2012-13: Mechi 57 Mabao 7
Brazil: Mechi 28 Hajafunga.





VIDEO: Mabao matamu ya Juan Mata Chelsea 
VIDEO: Bao tamu la David Luiz dhidi ya Basle katika Europa League








Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post