Serikali imetupiwa lawama kwa kushindwa kudhibiti matukio ya kijangiri yanayoendelea kushamiri katika hifadhi mbalimbali hapa nchini.
Hayo yamesemwa na waziri kivuli maliasili na mazingira PETER MSIGWA wakati akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake, kutokana na vitendo hivyo kushamiri na watu wengi kukamatwa wakiwemo askali polisi maafisa wapelelezi wanajeshi pamoja na viongozi ambao wananchi wanawaamini na kuwapa dhaman za uongozi.
Msigwa amesema kuwa tatizo hilo limekuwa kubwa nchini lakini cha kushangaza waziri mwenye dhamana bado analifumbia macho kwa kuwatetea wahalifu licha ya wapinzani kuwataja wahusika.
Msigwa amesema kuwa wahusika wakubwa katika vitendo hivyo ni watu ambao wananchi wanawategemea katika kulinda maliasili ya taifa lakini cha kushangaza wao ndio wanakuwa watuhumiwa nambamoja jambo ambalo linasikitiasha taifa.
Aidha ameongeza kwa kusema kuwa kwa bahati mbaya tumewapa watu dhamana ambao hawajui majukumu yao badala ya kulinda watu wao wapo katika masilahi yao binafsi.
hata hivyo amewaomba wananchi kushirikiana katika kuchagua viongozi watakaotunza maliasiri za nchi ili kuleta faida kwa nchi na wananchi kwa ujumla kuliko kuweka viongozi wasiojua wajibu wao na kusababisha uchumi wa nchi kushuka.
WAKATI HUO HUO........!.
Kutokana na vitendo vya ubakaji kushamiri katika mkoa wa Iringa ,Kamanda wa jeshi la polisi RAMADHANI MUNGI amekemea vikali vitendo hivyo na kusema kuwa ni makosa dhidi ya Binadamu.
Akizungumza,Kamanda Mungi amesema kuwa mtu yoyote anayefanya mapenzi na msichana au binti chini ya umri wa miaka 18 hata kama atakuwa amekubali kwa hiari yake bado atahesabiwa kuwa mbakaji.
Mungi amesema kuwa vitendo hivyo vinasababishwa na matatizo ya kisaikolojia hivyo watalamu wa saikolojia wanapaswa kulishugulikia suala hilo ili kusaidia kupunguza matukio kama hayo.
Aidha ameongeza kwa kusema kuwa kutokana na wananchi wengi kulalamika juu ya kuachiwa huru kwa watuhumiwa wenye makosa ya ubakaji, amesema kuwa ni haki yao kupewa dhamana kwa mujibu wa sheria na sio kwamba polisi wanafanya makusudi.
SOURCE: JIACHIE BLOG
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.