Katika article hiyo Josephine Masongo amejaribu kulinganisha hali ya mtu kuwa kufanikiwa kuwa socialite katika jamii flani kwa kipindi cha miaka ya nyuma na kipindi hiki tunachoishi, ambapo ameonesha kuwa katika miaka ya nyuma mtu kufahamika kama mtu anaejulikana sana kwenye jamii inayokwenda na wakati (socialite) ilimbidi afanye kazi nzuri katika jamii n.k, lakini kwa kipindi hiki ni tofauti.
Mwandishi huyo amefunguka kuwa katika kipindi hiki watu wanajipatia umaarufu zaidi kwa kupost picha za utupu kwenye mitandao ili waongelewe sana katika jamii na kumtaja Huddah Monroe, Paris na Kim Kardashian kama mfano wa wanaozungumzwa sana kutokana na kuteka media kwa tabia hiyo na sio vinginevyo.
Ametaja mbinu za kuonekana kwenye jami zaidi zinazotumiwa ni kama kupiga picha za utupu na kuzipost, kujitahidi kuonekana kwenye camera, kutengeneza drama na story za utata hasa kwa kuanzisha ugonvi kupitia mtandao wa twitter na mtu kisha radio na TV zitakutafuta kukuuliza kwa nini umeamua kutweet vile.
Article hiyo imepambwa na picha ya Huddah, hali inayoonesha kuwa ilimlenga yeye pia.
Article hiyo imemuudhi Thee Boss Lady Huddah Monroe na kutoa matusi kwa mwandishi huyo na kuamua kujibu kupitia akaunti yake ya twitter.
SOURCE: LEOTAINMENTTZ
Tags
HABARI ZA WASANII