Mwili wa mtoto ukiwa umefunikwa na kitenge na kutelekezwa kwenye kiti
Ezekiel Kamanga
Vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na wanawake jijini mbeya vimeendelea chukua sura mpya baada ya dereva wa daladala jijini humo kumzalisha mwanafunzi wa Masomo ya jioni kituo cha Juhudi kilichopo Ilomba.
Tukio hilo limetokea hivi karibuni eneo la mama John Mtaa wa Ihanga Kata ya Ilomba ambapo dereva wa daladala aliyefahamika kwa jina la Aswile Mwalukoba (45 ) kutelekezewa mtoto wa miezi saba ambaye alikwisha fariki baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Akizungumzia tukio hilo Mwenyekiti Mtaa huo Ndugu Emanuel Mwasibata amesema kuwa mgogoro huo umetokana na dereva huyo kugoma kuuzika mwili huo kwa kile alichodai kuwa hivi sasa haishi na binti huyo kwa muda mrefu sasa.
Kwa upande wake binti huyo aliyefahamika kwa jina la Calorina Kyando amedai kuwa kitendo cha yeye kuuchukua mwili wa mtoto huyo hadi kwa baba yake unatokana kutelekezwa na bwana huyo kisha kupigwa mara kwa mara na kusababishiwa ulemavu wa sikio la kushoto baada ya kung’atwa na mwanaume huyo.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.