AIRBUS LAPATA AJALI ENEO LA MASEYU, MOROGORO

clip_image001Basi la Airbus likiwa safarini. Moja ya mabasi hayo limepata ajali jioni hii

ABIRIA 23 waliokuwa wakisafiri na basi la Air Bus linalofanya safari zake kati ya Tabora na Dar wamejeruhiwa wanne kati yao vibaya baada ya basi hilo kupinduka eneo la Maseyu, mjini Morogoro.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotangazwa na Radio One ni kwamba basi hilo lilipinduka kutokana na mwendo kasi wakati likijaribu kuyapita malori na kupoteza muelekeo kabla ya kupinduka.

Taarifa hizo zinasema kuwa, majeruhi wameumia vibaya maeneo ya kichwani, kifuani na miguuni na wamekimbizwa hospitali ya Mkoa wa Morogoro, huku wanne akiwemo dereva wa basi hilo wenyewe wakiwahishwa jijini Dar es Salaam katika hospitali ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Kati ya abiria hao waliojeruhiwa 13 wamelazwa hospitali hiyo ya mkoa wa Morogoro, na kwamba taarifa zaidi zinaendelea kufuatiliwa ili kujua kinachoendelea, ingawa mpaka sasa hakuna kifo chochote kilichoripotiwa.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post