WAJANJA WAUGEUZA MSIBA WA NGWEA DILI, HIKI NDO WANACHOKIFANYA

clip_image001WAKATI wapenzi wa Bongo Fleva wakiwa kwenye majonzi kufuatia kifo cha msanii Albert Mangwea ‘Ngwea’ kilichotokea Mei 28, mwaka huu, kumeibuka kundi la watu wanaotumia mwanya huo kuvuna fedha kwa kutengeneza fulana zenye picha ya marehemu.
Akizungumzia juu ya wajanja hao akiwa maeneo ya Mbezi jijini Dar juzikati, msemaji wa kamati ya mazishi, Adam Juma alisema amechukizwa na kundi hilo la watu linalouza fulana hizo kwa masilahi yao binafsi.
 “Tutawachukulia hatua wote watakaobainika kuprinti t-shirt bila kuleta fedha kwenye msiba. Ni kinyume cha taratibu, sisi tuliandaa t- shirt maalum kwa utaratibu maalum wa kuisaidia familia na si vinginevyo,” alisema Juma.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post