Unknown Unknown Author
Title: TIGER WOODS KINARA KWA KUINGIZA FEDHA NYINGI - BECKHAM AENDELEA KUWAKIMBIZA MESSI NA RONALDO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Tiger Woods amerudi kwenye uongozi wa wanamichezo wanaongoza kutengeneza fedha nyingi kwa mwaka kwa mujibu wa jarida la Forbes la Marekani. ...

clip_image002Tiger Woods amerudi kwenye uongozi wa wanamichezo wanaongoza kutengeneza fedha nyingi kwa mwaka kwa mujibu wa jarida la Forbes la Marekani.
Mcheza gofu huyo namba namba moja duniani mwenye miaka 37, alikuwa akishika nafasi ya tatu katika listi iliyopita, lakini safari hii mmarekani huyo ameingiza kiasi cha  $78.1m (£50.7m) ikatika kipindi cha miezi 12 kutoka 1 June 2013 baada ya kuingia kwenye mikataba kadhaa ya matangazo na hivyo kuongeza mapato yake.
Mcheza Tennis Roger Federer ameibuka na kushika nafasi ya pili rose kwa kuingiza $71.5m (£46.4m) wakati mwanasoka aliyestaafu David Beckham, amebaki nafasi ya nane.
Taarifa hiyo ya Forbes inaonyesha kwamba Beckham, wakati akiwa mmoja ya wanamichezo maarufu zaidi duniani kote, alishika nafasi ya nne katika wale waliotengeneza fedha nyingi kupitia mikataba ya matangazo.
Nahodha huyo wa zamani wa England alitangaza kustaafu kucheza soka baada ya kushinda ubingwa wa ligue 1 na Paris Saint Germain, aliongeza mapato yake mpaka kufikia $47.2m (£30.6m), lakini fedha hizo alizotengeneza kupitia mikataba ya biashara ilimfanya awe nyuma ya Woods, Federer na mwanagofu Phil Mickelson, na mcheza basketball LeBron James.
Beckham bado anabakia mwanasoka anayetengeneza fedha nyingi zaidi, akifuatiwa na winga wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ($44m/£28.6m) na mpinzani wake mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi ($41.3m/£26.8m), ambao wanaitimiza top 10.
Mcheza gofu wa Ireland  Rory Mcllroy alitengeneza $29.6m (£19.2m) na kushika nafasi ya 21, wakati dereva wa Formula 1 Lewis Hamilton alifuatia kwenye nafasi ya 26 akiwa na $27.5m (£17.6m).
Mshambuliaji wa Manchester United na England Wayne Rooney alishika nafasi ya 24 akiingiza $21.1m (£13.7m), huku nahodha wa England na Liverpool Steven Gerrard akimfuatia $17.2m (£11.2m).
Boxer Floyd Mayweather aliyeshika nafasi ya kwanza mwaka uliopita ameshuka mpaka nafasi ya 14 kwa mapato ya $34m (£22.1m) kupitia mapambano yake.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top