Timu ya mpira wa miguu ya Taifa 'Taifa stars' leo wametoka sare ya bila kufungana na timu ya taifa ya Sudan katika mchezo wa kirafiki uliochezwa katika jiji la Adis Ababa nchini Ethiopia.
Taifa stars imejipima nguvu na Sudan ikiwa sehemu ya maandalizi ya kuwakabili Moroco katika mchezo wa kusaka nafasi ya kushiriki kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazili.
Katika mchezo wa leo wa kirafiki uliokwisha kwa sare ya bila kufungana Stars walikosa huduma ya beki wa kulia Erasto Nyoni aliyeumia katika mazoezi ya timu hiyo nchini Ethiopia na nafasi yake hii leo alichezeshwa na Nadir Haroub ;Canavaro' na katika kipindi cha pili alichezeshwa Vicent Barnabas.
Nnje ya Nyoni Stars walikosa pia huduma ya washambuliaji wake wanao cheza katika timu ya TP Mazembe ya DR Congo, ambapo leo walikuwa nchini Msumbiji wakiiwakilisha timu yao katika mchezo wa kombe la shirikisho.
Samatta na Ulimwengu watajiunga na Stars jijini Casablanca, Morocco teyari kuwakabili Morocco mwishoni mwa juma.