SHILOLE AFUNGUKA KUHUSU VIFO VYA WASANII "WASANII TUTAZIDI KUPUKUTIKA MAANA TUNAROGANA SANA..

clip_image002MSANII wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amefunguka kuwa, suala la wasanii wa muziki kurogana linamuumiza kichwa kiasi cha kufikiria kuachana na kazi hiyo.

Akiongea na mwandishi wetu pasipo kuwataja  wabaya  wake, Shilole alisema hivi sasa ‘kesi’ za wasanii kurogana zimeshika kasi kuliko siku za nyuma na anashindwa kuelewa ni kwa nini watu wanamuasi Mungu kwa kuendekeza ushirikina.
“Kwa staili hii wasanii tutazidi kupukutika, kuna wakati huwa nafikiria hata kuachana na muziki maana tunarogana na namuomba Mungu usiku na mchana hata kabla ya kupanda stejini kwani hali ni tete,” alisema Shilole.

SOURCE: PETERSANGA BLOG

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post