Unknown Unknown Author
Title: RIWAYA: SITAISAHAU FACEBOOK SEHEMU YA NNE
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
RIWAYA: SITAISAHAU facebook MTUNZI: Emmy John Pearson SIMU: 0654 960040 SEHEMU YA NNE “Isabela…. .” “Abee!!.” Niliitika. “Kampuni yangu ime...

clip_image001RIWAYA: SITAISAHAU facebook
MTUNZI:
Emmy John Pearson
SIMU: 0654 960040

SEHEMU YA NNE
“Isabela…. .”
“Abee!!.” Niliitika.
“Kampuni yangu imeamua kufanya kazi na wewe. Kama nilivyokwambia awali tulipowasiliana kwa njia ya simu”
“Nashukuru sana Dokta.” Nilishukuru, hakujali hilo akaendelea
“Unauchukia umasikini?.”
“Nauchukia kuliko niavyoweza kujielezea.” Nilisisitiza.
“Na…ok!...anyway..unaenda sana kanisani.”
“Aaah!! Kiukweli ni mara chache chache.”
“Kwa nini?.”
“Aaah!! Mambo huwa yanakuwa mengi sana.”
“Ok!! Achana na hayo…Isabella kazi uliyopata hapa ni kazi nyepesi kama ukipenda iwe nyepesi na ngumu pia iwapo utpenda iwe ngumu na kila mwezi itakuingizia si chini ya shilingi za Tanzania kwenu milioni sita laki sita na elfu sitini na sita kila mwezi.” Alizungumza Dokta bila wasiwasi kana kwamba alikuwa akitaja shilingi lakini moja tu, alimanusura nipoteze fahamu. Mwili ukawa wa baridi. Nikajaribu kujishtua huenda ninaota, haikuwa hivyo. Hali ile ilikuwa halisi.
Nilikuwa Zambia na nilitangaziwa dau hilo kubwa. Mwanzoni nilidhani ni mshahara wa milioni mbili sasa zimefika sita!! Mara tatu zaidi!!
“Tukiachana na hilo na mshahara, Unawazungumziaje wanaume kwa ujumla?.” Davis hakujali ule mshtuko wangu akanitupia swali jingine, bila shaka milioni sita kwake si lolote si chochote.
“Wanaume? Aaah!! Kiaje labda” Nilimuuliza huku nikifinya finya mikono yangu kuonyesha heshima.
“Vyovyote vile lakini hasahasa katika ngazi ya mapenzi.”
“Viumbe waongo, wasiokuwa na huruma, wanyanyasaji na…”
Nilishindwa kuongea nilikuwa nimemkumbuka John, mwanaume aliyeamua kuachana nami kisa sina pesa. Sasa hapa nazungumzia juu ya kupata pesa.
“Ok! Kila msichana husema hivyo, haya labda ukiambiwa uwape adhabu utatoa adhabu gani kwao.”
“Dah!! Sijui watoweke duniani…aaah!! Sijui ila nawachukia wanaume wenye tabia hii.” Nilimjibu huku nikilegeza koo kwa kugida funda mbili za juisi ile. Ilikuwa tamu sana. sijui tunda gani lile!!! Sijawahi kuinywa nikiwa Tanzania.
“Ok kikubwa hutakiwi kuwachukia wanaume, huoni kuwa utawachukia wazazi wako, na kila baba utamchukia. Mbaya zaidi hata anayetaka kukuajiri mbele yako hapa utamchukia….si unaona kuwa haupo sahihi!!!”
“Ni kweli..usemayo, ujue hasira Davis, wanaume wanakera sana. Unaweza kumpenda lakini aaargh!! Wanahitaji elimu wanaume na wasichana pia…”
“Safi sana…kumbe kazi utaiweza kabisa lakini lazima kwanza ubadili kwanza mawazo yako hayo ya kuombea wanaume watoweke. Lengo la kampuni yangu mimi ni kuwabadili wanaume kuacha na mfumo huo wa unyanyasaji na pia kuwafunza wanawake kuepukana na vishawishi vya wanaume wadanganyifu. Kwa mtazamo huu wa maneno yako mimi na wasaidizi wangu tunaamini kuwa utaweza kutuwakilisha vyema katika nchi yako. Ukimuelimisha msichana mmoja kwa siku basi ujue umeielimisha jamii kubwa sana.” Aliongea kwa umakini mkubwa huku akiwa amenikazia macho. Nilikwepesha kutazamana naye.
“Nitaweza hata usitie shaka.” Niliikubali kazi. Zikaangushwa karatasi nne mezani nikasaini mkataba mnono. Mkataba ambao nilijutia kwa muda mrefu kuusaini bila kuusoma, nilichoangalia ni masilahi binafsi hasahasa katika suala la mshahara.
“Baadaye kidogo pesa ya utangulizi itaingizwa katika akaunti yako.” Alimaliza Dokta.
“Tunaweza kuzunguka zunguka kidogo uitazame ofisi yangu. “ Lilikua ombi la Dokta nikakubaliana nalo. Na nisingeweza kulipinga katu.
Tulizunguka kona tofauti tofauti. Nilikuwa nikimtazama Davis kwa kuibia ibia na yeye pia alifanya hivyo. Yale mawazo ya kumfanya awe mpenzi wangu yakawa yananisumbua akili nilitamani kumwambia lakini mdomo ukawa mzito. Kwanza angeniona sina msimamo, nimetoka kuwalaani wanaume na sasa nimtamkie kuwa napenda awe wangu!! Hapana hata!! Nitajidhalilisha katika nchi za kigeni. Hapo hapo nikagundua kuwa kitend hicho kinaweza kunifukuzia bahati niliytoipata ya kulipwa mshahara wa milioni sita!! Nd’o kwanza nilikuwa na miaka ishirini na tatu. Bahati iliyoje.
Lakini licha ya kuwaza yote hayo bado wazo la kuwa mchumba wa Davis na hata mke kama inawezekana halikunitoka kichwani.
Laiti kama nikiwa naye!! Hata hii ofisi pia itakuwa mali yangu!! Niliwaza.
*****
MWANZA
Ulikuwa usiku wa kipekee sana kwangu, ndio kwanza nilikuwa nimerejea jijini Mwanza, kwa usafiri bora wa ndege. Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu. Sijui niseme mara ya pili!! Maana mama alinihadithia kuwa nilipokuwa mtoto niliwahi kupanda ndege!!!
Baada ya kushuka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam bila kuwa na wa kunipokea sasa hapa uwanja wa ndege wa Mwanza nilihitaji mtu fulani ajue kuwa nimekuja na ndege!! Huyo mtu ni nani kama sio John!!!
Nilimwomba John afike kunipokea. Nilifanya hayo makusudi ili kumkomoa kwa ubaya alionifanyia. Ubaya wa kuniacha na kuwa na mahusiano na msichana mwingine. Kwa kuniona nikishuka katika ndege lazima tu angeumia, na huu kwangu ungekuwa ushindi mkubwa!!
Ni kweli John alikuwa amenitenda vile lakini John bado alikuwa moyoni mwangu. Nilikuwa nampenda sana John. Walikuwepo wanaume wengi lakini nafasi ya John bado nilikuwa sijaona wa kumrithisha. John alikuwa ni mwanaume ambaye nilidumu naye kwa muda mrefu sana!!
John aliposikia nakuja na ndege hakusita kukubali kuja kunipokea. Labda ili athibitishe kwamba kweli nimekuja na ndege ama la. John alinipokea huku akinipapatikia, niliifurahia hali hiyo ya kuonekana kuwa mimi ni mtu kati ya watu. Nilikiweka kando Kiswahili kwa muda wakati nikiagana na mzungu mmoja ambaye nilipanda naye ndege kutokea Dar es saalam, hata baada ya kuagana naye niliendelea kubonga kiingereza. Kisha nikampatiua ‘Business card’ wakati wa kuagana!! Business card hizo alinitengenezea Davis kama kukaribishwa rasmi katika kampuni yao. Macho yalimtoka John, nikafurahia tena kimyakimya.
Tulichukua taksi iliyotufikisha katika hoteli yenye hadhi ya juu ya La kairo jijini Mwanza tukajipatia chumba. Chumba cha bei ya juu kabisa!! Sikuwa na wasiwasi kuhusu pesa!!
Wakati huo John tayari alikuwa amemdanganya mpenzi wake wa wakati huo Jesca kuwa hatarejea chuoni siku hiyo kwa kuwa kuna rafiki yake anaumwa. Ameenda kumsalimia. Wanaume bwana!! Yaani wakiona sehemu fulani tu ina masilahi wapo tayari kuwa hata na wapenzi kumi kwa wakati mmoja!! John alikuwa amechachawa na muonekano wangu mpya.
Usiku majira ya saa nne, tayari tulikuwa tumelia sana baada ya kukumbushiana yaliyopita. John akaniomba msamaha kwa yote yaliyowahi kutokea baina yetu, nami sikusita kumsamehe maana nafsi yangu ilikiri kuwa nilikuwa namuhitaji bado!!
Kilichofuata hapo ni kurejesha hisia za zamani na kuanza kushambuliana, kila mmoja akijitahidi kuamsha hisia za mwenzake kwa mbinu zote lakini zisizoleta maumivu lakini badala yake furaha!!, baadaye kidogo. Vita!!!
Vita ya miili. Kila mmoja akitamani kuibuka mshindi, hapakuwa na mwamuzi. Wakati vita hiyo ikiendelea ndipo ikaanza kusikia kama sauti ikiniongelesha kwa kabila kama kihehe vile, lakini sikuweza kuielewa lakini niliwahi kuisikia mahali. Ni kweli niliwahi kuisikia mahali, lakini sasa sikuwa nakumbuka ni wapi. John alikuwa bize, huenda alikuwa akifurahia peke yake tendo alilokuwa akifanya. Nilitamani kumwambia John azisikilize zile sauti lakini hakuweza kunisikia alikuwa ulimwengu mwingine.
John alipokoma, na sauti zile nazo zikatoweka. Ni kama vile zilikuwa kando ya dirisha zikitusemesha ama zikinisemesha.
“John walikuwa wanasemaje?.”
“Nani?. Hao wahudumu ama.?” Aliuliza kwa utafiti.
“Hapana!!!anyway acha ilivyo.” Nilimaliza mjadala.
John hakuuliza zaidi.
Nilielekea bafuni kujisafisha, kisha nikarejea tena pale kitandani. John alikuwa amesinzia. Sikuwa na hamu naye tena bali nilizitafakari zile sauti zilikuwa zikisema nini.
Lakini kama John , hajazisikia basi hakuna sauti yoyote!!! Nilijipa moyo. Henda hata ni utamu wa kilichokuwa kinatokea ndio ulioniletea balaa lile la kusikia sauti za kihehe. Nikatabasamu kisha nikajiunga na John kulala!!
Asubuhi John alikuwa wa kwanza kuamka. Aliingia maliwatoni akajisafisha na kuniamsha. Nami nikafanya kama alivyofanya kisha tukaondoka. Nilimpatia John shilingi elfu hamsini kwa ajili ya nauli yake!! John alikodoa macho asiamini anachokiona!! Kisha akaelekea alipopajua nami nikaelekea chuoni. Kilichotokea ilikuwa siri yetu wawili, na siri ile kama ingedumu basi tungeendelea kuwa tunafaidi
Zile sauti nilizozisikia usiku ule sikuzikumbuka tena. Nilichokumbuka ni kwamba mimi na John tulikumbushia enzi.
******
Sikuweza kujua ilikuwa ni saa ngapi, lakini niliamini ilikuwa ni usiku tena usiku sana. Kuna sauti zilikuwa zimezungumza nami, tena kwa lugha ninayoielewa, zilikuwa sauti zenye furaha sana.
Nikiwa bado natafakari sauti hizo zilizungumza nini na mimi. Mara simu yangu iliita. Alikuwa ni rafiki yangu wa darasani. Nikajiuliza kulikoni usiku kiasi kile, sasa niliweza kuona katika simu ilikuwa saa sita usiku. Nikaipokea simu.
“Isabella, Isabella….Jenipher jamani. Jenipher!!”
“Amekuwaje tena. Eh!! Nambie.”
“Jenipher yupo hoi hospitali hapa.” Alijitahidi kuongea bila taharuki lakini alisikika akitetemeka. Baada ya pale hata kabla sijamjibu, simu yake ilikatika. Nilipojaribu kumpigia hakupatikana. Nikajilazimisha kulala, huku nikiamini kuwa lile ni tatizo la kawaida tu mwanafunzi kuugua na kisha kupelekwa hospitali.
Wasichana kwa kukuza mambo, hatujambo!! Nilijisemea kisha nikauchapa usingizi.
Asubuhi palipopambazuka, taarifa ilikuwa nyingine, taarifa ya kushtua nafsi!! Jenipher msichana aliyekuwa akiishi na huyo rafiki aliyenipigia usiku uliopita.alikuwa amefariki baada ya jitihada za madaktari kugonga mwamba kumuokoa.
Ilikuwa habari ya kusikitisha sana kwani kilikuwa kifo cha ghafla mno. Mbaya zaidi alikuwa mtoto pekee katika familia yao. Huzuni kwa baba kilio kwa mama mzazi!!!
Sikuzikumbuka tena zile sauti za usiku ule zilikuwa zinasema nini na mimi. Sauti za furaha, Sasa nikawa nawaza juu ya msiba huo!! Msiba wa ghafla!!
Msiba wa Jenipher!!
Nilipowaza jina hilo mara nikakumbuka kama vile zile sauti zilitaja jina Jenipher!! Nilijitahidi kukumbuka palikuwa na maneno gani mengine kabla ya neno hilo Jenipher lakini sikuweza kukumbuka chochote. Nikajihisi kuwa huenda ni msiba unaivuruga akili yangu na kuwaza mambo na sauti zisizokuwepo.
Lakini mara mbili? Kwa nini niwaze mara mbili sasa!! Sauti za kihehe si kihehe, kibena si kibena!! Kazi kwelikweli lakini sauti hizi zimetja jina Jenipher…
Au ni ile sauti ya rafiki aliyenipigia mimi nachanganya na hizo sauti za kibena?? Nilijiuliza na kisha kuegemea katika pointi hiyo kama jibu sahihi!!!

***Je huu msiba unahusiana na sauti za maajabu?
****Sauti hizo zinatoka wapi? Na je? Ni kweli zilitaja jina Jenipher?? Kwanini zimtaje??
***Mkataba alisaini Isabela ni kweli mkataba wa kazi??

MAONI yako ni ya muhimu sana…ITAENDELEA…..i!!!

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top