RATIBA ya Ligi Kuu ya England imetoka na mechi ya kwanza ya David Moyes nyumbani kama kocha mpya wa Manchester United itakuwa dhidi ya Cheslea yenye kocha mpya pia, Jose Mourinho.
Mabingwa hao wa Ligi Kuu, United watakuwa na mwanzo mgumu katika ligi hiyo msimu ujao 2013-14 wakisafiri kuwafuata Liverpool na Manchester City ndani ya mechi tano za mwanzoni.
United itaanza na mabingwa wa Kombe la Ligi, Swansea Agosti 17, kabla ya kurejea nyumbani kumenyana na Mourinho na Chelsea yake Old Trafford wikiendi inayofuata. Mechi na Liverpool itafuatia Agosti 31 kabla ya kuifuata City katika mchezo wa tano wa msimu, Septemba 21.
MECHI ZA UFUNGUZI LIGI KUU ENGLAND (AGOSTI 17)
Mabingwa: Man United tayari kutetea taji chini ya David Moyes
Anaanza na moto: Moyes atakutana na Chelsea na Liverpool katika mechi zake za ufunguzi
MECHI ZA KUFUNGA MSIMU LIGI KUU (MEI 11)
Zilizopanda:Hull (kushoto) na Cardiff (kulia) zote zitacheza nyumbani mechi za kufunga msimu