Naibu waziri wa malisaili na utalii tanzania NYARANDU amesema hali ya ujangili Tanzania ni kubwa, jambo ambalo linahatarisha usalama wa Taifa.
Hayo ameyasema leo wakati wa akifungua kikao cha wadau wa ulinzi wa malisaili mikoa ya nyanda za juu kusini mwa Tanzania mkoani hapa.
NYARANDU amewataka wananchi wanaomiliki siraha kinyume na taratibu kuzisalimisha mapema na wanaojihusisha na ujangili kuacha maramoja vitendo hivyo.
kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Iringa CHRISTINE ISHENGOMA amesema anaamini kuwa kikao hicho kinachofanyika kwa siku mbili kitatoa suluhisho la kukomesha vitendo vya ujangiri katika ukanda huu.
kikao hicho cha wadau wa ulizi wa maliasili mikoa ya nyanda za juu kisini kimeandaliwa na mradi wa kuboresha mtandao wa maeneo yaliyo hifadhi kusini mwa tanzania (SPANEST)kikao hicho kimehudhuliwa na wakuu wa mikoa ya mbeya,njombe,dodoma na mwenyeji iringa, wengine ni mkurugenzi wa TANAPA na wakuu wa wilaya na wadau wengine.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.