Unknown Unknown Author
Title: MKUU WA MKOA ANENA NA WAENDESHA BODA BODA MKOANI LINDI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mwenyekiti wa chama cha Madereva Boda Boda na Bajaji Manispaa ya Lindi Rajabu Bahari akiongea neno wakati wa kikao na Mkuu wa Mkoa wa Lindi,...

DSC05024Mwenyekiti wa chama cha Madereva Boda Boda na Bajaji Manispaa ya Lindi Rajabu Bahari akiongea neno wakati wa kikao na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Hapo jana Uwanja wa IluluDSC05035Mkuu wa mkoa wa Lindi Ndg Ludovic Mwananzila akiongea na Waendesha Bodaboda na Bajaji Mkoani Lindi katika Kikao cha pamoja kilichofanyika Jana Uwanja wa ilulu.DSC05030Mh. Meya wa Manispaa ya Lindi Ndg Frank Magari akiongea na Waendesha Boda Boda na bajaji wa Manispaa ya Lindi Hapo jana katika Kikao cha pamoja na Mkuu wa Mkoa wa LindiDSC05031Al-Ustadhi Anafi Abdallah akisoma risala fupi kwa Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa Ndg Ludovic Mwananzila.DSC05036Waendesha Bodaboda na bajaji wakifuatilia kwa makini mazungumzo katika kikao cha pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Lindi ndg Ludovic Mwananzila Hapo jana uwanja wa Ilulu.DSC05045Mkuu wa Mkoa akisalimiana na wanachama wa Umoja wa Waendesha Bodaboda na Bajaji Mkoa wa Lindi, Hapo Jana

Na Mwandishi wetu, Lindi

Mkuu wa mkoa wa Lindi Ndg Rudovic Mwananzila ameketi katika kikao cha pamoja na waendesha boda boda na Bajaji mkoani hapa na kuongelea mambo mbali mbali ya maendeleo na uchumi katika mkoa na kuwataka kuwajibika kwa moyo na uaminifu mkubwa katika jamii kwani wao wako karibu sana na jamii kutokana na kazi yao waifanyayo ya kutoa huduma ya usafiri mjini hapa hivyo wanatakiwa kuonesha hali ya nidhamu na ueledi katika kazi yao

Aliyasema hayo hapo Jana wakati wa kikao cha pamoja na chama cha Madereva Boda Boda na Bajaji mkuani lindi, aidha aliwataka uongozi wao kukifanya chama hicho kukua kiuchumi na kusisitizia jambo hilo alitoa ahadi ya Kuwachangia Tsh 2,000,000.00 katika kutunisha mfuko wao, aidha katika taarifa ya awali iliyosomwa na AL Ustadh Anafi Abdallah walimshukuru mkuu wa mkoa kwa kuwatambua na kuweza kuwaita na kuzungumza nao ili kueleza matatizo na changamoto wanazozipata katika shughuli zao za kazi.

Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Mh Meya wa Lindi Mjini Ndg Frank Magari pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ambao nao kwa pamoja walilidhia kutoa mkopo wa kiasi cha Tsh 1,000,000.00.

Katika mambo yaliyo weza kuchukua ukubwa wa kikao hicho ni kuwahimiza wakazi wa mji wa lindi kufanya shughuli mbalimbali ili kukuza uchumi wa mkoa kwani kukaa vijiweni hakusaidii pia mkuu wa mkoa aliwapongeza kwa kuwa watulivu na akawataka kutoshawishiwa na mto yeyote kujiingiza katika vurugu za uvunjifu wa amani kwani amani ikitoweka hapatokuwa na Kazi hivyo kudhorotesha Uchumi wa mkoa na kuwaomba kuwafichua wale wote wanao jaribu kuchochea vurugu mkoani hapa.

Aliongeza kuwa Wanchi wajitokeze kuomba kazi katika makandarasi wa ujenzi wa bomba la Gesi linalotarajia kujengwa hivi karibuni kutokea Mtwara kwenda Dar es Salaam, aliwatoa hofu wanachama hao na kuwaambia hakutokuwa na Tatizo lolote kwani ulinzi utakuwepo masaa ishirini nanne hivyo hakutokuwa na tatizo lolote.

Wanachama hao walimuhakikishia Mkuu wa  mkoa kuwa wao si wagomvi na hawawezi kujiingiza katika vurugu zozote kwani zitaathiri kazi zao na hivyo kuwafanya wakose kipato na kumuomba mkuu wa mkoa kufikisha kiliochao kwa RPC kuhusu askari wa Barabarani kuwasumbua kila mara.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top