MANCHESTER UNITED WANATAKA KUKAMILISHA DILI LA RONALDO KABLA YA MECHI YA HESHIMA YA RIO FERDINAND

clip_image002MANCHESTER UNITED wana mtihani mkubwa katika vita ya kushinda saini ya Cristiano Ronaldo.
Mabingwa wa Premier League wana matumaini ya kumsaini Ronaldo kwa ada ya £65million — na kukamilisha usajili mkubwa kabisa katika historia ya soka la England.
United wanataka kumtambulisha Ronaldo mwezi August tarehe 8 na kumchezesha kwenye mechi ya kumshukuru Rio Ferdinand kwa kuitumikia United dhidi ya Sevilla siku inayofuata.
Lakini Ronaldo mwenyewe jana usiku alinukuliwa akisema bado anatzamia kukubaliana na Madrid juu ya mkataba mpya.
Lakini wawakilishi wa Ronaldo wametoa masharti magumu kwa Real, wakihitaji kiasi cha £35m kwa mwaka kama mshahara pamoja na haki zote za taswira yake.
lakini mpaka sasa inasemekana Madrid wapo tayari kutoa kiasi cha £30m kwa mwaka na asilimia 60 ya haki za taswira yake.
Mpango wa United ni kumlipa Ronaldo, 28, mshahara wa £300,000 kwa wiki na kumfanya kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi zaidi kwenye soka la England.

Inaeleweka kwamba mikutano isiyo rasmi ya pande zote 3 imekuwa ikiendelea kwa kipindi cha mwaka sasa.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post