Unknown Unknown Author
Title: KIKOSI MAALUM CHA KUPAMBANA NA UJANGILI TANAPA CHAHITIMU MAFUNZO RUAHA NATION PARK
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akikagua gwaride la kikosi maalum cha kupambana na ujangili katika ...

clip_image003Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akikagua gwaride la kikosi maalum cha kupambana na ujangili katika hifadhi za taifa wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika mbuga ya Ruaha kandokando ya mto Ruaha.

Wakipewa  mafunzo hayo na  wakufunzi Martin Mthembu  kutoka taasisi ya African Field Rager Training Services ya Afrika kusini na Genes Shayo ambaye pia ni Mhifadhi TANAPA, kikosi hicho maalum cha TANAPA kilikuwa na askari 20 wamehitimu mafunzo hayo askari  19 moja hakufanikiwa kumaliza mafunzo kwa sababu za kiafya, Kivutio kilikuwa kwa askari mwanamke pekee katika kikosi hicho Aikandaeli Lema ambaye aliweza kufanya mafunzo kwa kiwango cha juu bila kuwa na tofauti yoyote kiutendaji ya kijinsia ameweza kufanya mafunzo yote magumu na kulenga shabaha kwa kiwango cha juu kabisa alimwelezea mkufunzi wa mafunzo hayo Martin Mthembu  kutoka Afrika Kusini na akampa sifa na pongezi nyingi kwa uwezo wake kama mwanamke.

PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-RUAHA NATION PARK 3Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akirejea meza kuu mara baada ya kukagua gwaride hilo katika ufungaji wa mafunzo hayo 4Kikosi hicho kikitembea kusonga mbele tayari kwa kutoa heshimza zao kwa mgeni rasmi. 6 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akipokea heshima kutoka kwa kikosi hicho wakati alipofunga mafunzo rasmi ya kukabiliana na ujangili katika hifadhi za taifa kulia ni Adam Swai Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Iringa na kushoto ni Mkurugenzi wa Uhifadhi TANAPA  Martin Loiboki. 7Askari wahitimu wa kikosi hicho kushoto ni Frank Anthon Malema na Mwanamke pekee katika kikosi hicho Aikandaeli Lema wakisoma risala mbele ya mgeni rasmi wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo 8Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa katika hafla ya ufungaji wa mafunzo hayo 10Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo hayo askari Frank Anthon Malema kulia ni Mkurugenzi wa Uhifadhi TANAPA Martin Loiboki na kushoto ni Mkufunzi wa mafunzo hayo na mhifadhi TANAPA Genes Shayo 11Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo hayo askari Elisamehe Elisafi Mdeme kulia ni Mkurugenzi wa Uhifadhi TANAPA Martin Loiboki na kushoto ni Mkufunzi wa mafunzo hayo na mhifadhi TANAPA Genes Shayo 12Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akimpongeza John Kijazi  baada ya kupokea cheti cha kuhitimu mafunzo hayo 13Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akizungumza na wahitimu wa mafunzo hayo.14Martin Mthembu Mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka nchini Afrika Kusini akitoa maelezo kwa Allan Kijazi  Mkurugenzi wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA  wakati akikagua eneo maalum la kulenga shabaha katika ufungaji wa mafunzo hayo kulia ni Dr. Christopher Timbuka mhifadhi mkuu wa Ruaha Nation Park.

CREDIT TO FULLSHANGWE BLOG

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top