Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, amelazwa tena hospitalini Pretoria baada ya kukimbizwa hapo usiku wa jana. Mandela ambaye ana umri wa miaka 94 sasa anasumbuliwa na ugonjwa wa mapafu. Msemaji mkuu wa masuala yanayowahusu wakuu wa nchi Afrika kusini,Mac Maharaj amesema safari hii Mzee Madiba anaumwa zaidi na hali yake ni yenye utata zaidi.
Pamoja na kwamba Mandela aliachia nafasi ya uraisi zaidi ya miaka kumi iliyopita, dunia bado inamhusudu na kumkumbuka kama mfano mzuri wa kusamehe na kufanya maamuzi magumu kwa manufaa ya nchi badala ya kuweka mbele masilahi binafsi kama ambavyo viongozi wengi duniani (na hususani barani Afrika) wamekuwa wakifanya.
Kabla ya kutwaa madaraka ya Urais, Mandela alitumikia jela miaka 27 wakati wa vuguvugu kali la kupinga ubaguzi wa rangi nchini humo.
BC inaungana na kila mtu anayemtakia afya njema Mandela kumtakia uponaji wa haraka. Get Well Soon Madiba…Mandela na mkewe Graca Machel, wakati wa ufunguzi wa fainali za Kombe la Dunia Soka mwaka 2010
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.