Na: Fungwa K, Lindi.
Kariakoo Fc imefanikiwa kutinga katika raundi ya Pili ya Mzunguko wa kumtafuta mshindi wa Ligi ya Mkoa baada ya kuibugiza timu ya Kilwa Fc magoli matatu kwa moja leo katika uwanja wa ILULU mjini Lindi na kuweza kuongoza kwa point 6 na magoli 6.
Nasoro kupama ndiye alikuwa wa kwanza kuipatia timu yake ya Kariakoo Fc bao la kuongoza, lakini bao hilo halikuweza kudumu kwani timu ya Kilwa ilijibu mashambulizi na kufanikiwa kusawazisha goli hilo. hadi kipindi cha kwanza kinamalizika scoreboard ilikuwa ikisomeka 1 – 1.Kipindi cha pili kilianza kwa timu ya Kariakoo kushmbulia langu la Kilwa nakufanikiwa kupata penalti baada ya beki wa kilwa kumchezea rafu mchezaji wa kariakoo ndani ya eneo la hatari. Kapten Anafi Jamvi aliweza kupiga penalti safi na kuifanya timu yake iwe mbele kwa goli mbili.
Mpira ulizidi kuwa mkali kwani Kilwa walikuwa wakitafuta nafasi ya kuweza kurudisha goli hizo lakini ma beki wa kariakoo waliweza kufanya kazi nzuri na kuweza kulinda lango lao. Salum Abdillah aliweka historia kwa maranyingine baada ya kufunga goli la tatu na kuiwezesha timu yake kuibuka kidedea leo hii.
Kwa matokeo haya Timu ya Kariakoo wameweza kuwa viongozi wa Kituo cha lindi hivyo anasubiri kucheza na Mshindi wa pili kituo cha Nachingwea, Kesho kutwa Kusini soccer itakuwa na kibarua kigumu katika kutafuta nafasi ya mshindi wa pili ambapo watashuka dimbani kucheza na Kilwa Fc ambao leo hii wamekosa point tatu kutoka kwa Kariakoo Fc.
Tags
SPORTS NEWS