Stand kuu ya mji wa lindi ilivyo tangu jana saa 2:00 mchana, abiria wakionekana kufanyamijadala ya hapa na pale wakiwa hawajui nini cha kufanya kukamilisha safari zao.
Mabasi takribani ma tano yanayofanya safari zako Dar – Lindi – Mtwara bado yamekwama mjini Lindi kutokana na ghasia zilizoanza jana mkoani Mtwara hadi kufanya kufungwa kwa barabara hiyo inayo unganisha mikoa miwili ya Lindi na Mtwara inaaminika vuruguhizo zimepelekea kuvunjwa kwa Daraja eneo la Mikindani Mkoani humo ambapo ni sehemu ya kiungo cha Mikoa hiyo.
Wasafiri watokao Dar kwenda Mtwara wanaendelea kusubiri hali ya usalama irudi na kuweza kuendelea na safari yao hiyo ambayo haijulikani ni wakati gani na ni Lini wataweza kukamilisha safari zao.Wasafiri wa maeneo mengine kama Nyangao, Ndanda na Masasi waendelea na safari zao japo taarifa zilizopatikana asubuhi ya leo hii zilieleza kuwa Barabara hiyo ilifungwa na wananchi katika eneo la Kiwalala Mkoa wa lindi kwa kile kilichosemwa ni shinikizo kwa jeshi la polisi kuwaachia wananchi waliokamatwa hapo jana, Blog hii imefuatilia nakubaini kuwa hakuna ukweli juu ya madai hayo na Usafiri unaendelea bila ya shaka yeyote,
Endelea kutembelea blog tutakujuza kadri tunavyopata taarifa.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.