Mwokozi; Frank Lampard aliifungia England bao la kusawazishaFuraha: Shane Long akishangilia bao lake
ENGLAND imetoka sare ya 1-1 na Jamhuri ya Ireland katika mchezo wa kirafiki usiku kwenye Uwanja wa Wembley.Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa William Collum wa Scotland, Ireland ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao ugenini, mfungaji Shane Long dakika ya 13, akiunganisha kwa kichwa krosi ya Seamus Coleman kutoka wingi ya kulia.
Frank Lampard aliwasawazishia wenyeji dakika 10 baadaye, yaani dakika ya 23 kuftaia kazi nzuri ya Daniel Sturridge ambaye aliambaa uipande wa kushoto wa box, kabla ya kummiminia krosi mfungaji, aliyemtungua kipa Glenn Whelan.
Ashley Cole alipewa kofia ya dhahabu baada ya kutimiza mechi 100 za timu ya taifa ya England leo.
Katika mchezo huo, kikosi cha England kilikuwa: Hart/Foster dk46, Johnson/Jones dk46, Cahill, Jagielka, Cole/Baines dkl54, Walcott, Lampard, Carrick, Oxlade-Chamberlain/Milner dk87, Rooney na Sturridge/Defoe dk33.
Ireland: Forde, Coleman, O'Shea, St. Ledger, Kelly, Walters/Sammon dk82, McCarthy, Whelan/Hendrick dk74, McGeady/McClean dk68, Long na Keane/Cox dk66.
Roy Hodgson akimkabidhi Ashley Cole kofia ya dhahabu kwa kutimiza mechi 100 EnglandStephen Kelly wa Ireland akimdhibiti Theo Walcott wa EnglandWayne Rooney akipiga shuti lililopaaNahodha wa England, Ashley Cole akivutwa jezi na Seamus Coleman wa IrelandShane Long wa Ireland akipambana na Gary Cahill wa EnglandFrank Lampard (kulia) akiisawazishia England
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.