Mwanafunzi wa Chuo Cha Ualimu Kasulu, mkoani kigoma Valerian Nickodemus Kamugisha akinyannyua kwa Furaha sehemu ya fedha Sh 100 Milioni alizoshinda katika droo kuu ya Promosheni ya Vodacom Mehala iliyomalizika hivi karibuni. Kamugisha amekabidhiwa fedha zake hizo leo jijini Dar es salaam na kuamua kuzifungulia akaunti katika benki ya NMB. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NMB Bw.Abdulmajid Nsekela na Mkuu wa Chapa Vodacom na Mawasiliano Kelvin Twissa.Mkuu wa Chapa Vodacom na Mawasiliano Kelvin Twissa akimtambulisha kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) mshindi wa Promosheni kuu ya Mahela iliyomalizika hivi karibuni Valerian Nickodemus Kamugisha (kushoto) wakati wa hafla ya kumkabidhi kitita chake cha zawadi ya sh. 100 Milioni iliyofanyika makao makuu ya NMB. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NMB Bw.Abdulmajid Nsekela.Valerian Nickodemus Kamugisha (katikati) akipokea kitita cha sh. 100 Milioni kutoka kwa Mkuu wa Chapa Vodacom na Mawasiliano Kelvin Twissa alizoshinda katika droo kuu ya Promosheni ya Vodacom MAHELA. Hafla ya makabidhiano imefanyika makao makuu ya benki ya NMB ambako mshindi huyo amechagua kufungua akaunti kuhifadhi fedha hizo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NMB Bw.Abdulmajid Nsekela.
Home
»
HABARI ZA KITAIFA
» HATIMAE MSHINDI WA PROMOSHENI YA VODACOM MAHELA AKABIDHIWA KITITA CHAKE LIVE.
About Author
JE, UNA HABARI, PICHA, TANGAZO, MAKALA NA USHAURI? USISITE KUWASILIANA NASI SIMU / WHATSAPP NAMBA 0625535420.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.