EXCLUSIVE: HIKI NDICHO ALICHOJIBU CHIDI BAADA YA KUPIGWA NA KALA PINA

clip_image002
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Chid Beenz, amesema watu wengi wanayafatilia maisha yake sababu yeye ni msanii mkubwa na ni star zaidi yao.
Chid ambaye masikani yake ni Ilala Flats jijini Dar, amesema kitendo cha watu kuwa wanamfatilia kwa yale au kile anachokifanya sababu yeye ni msanii mkubwa na wasanii wengine inabidi  wamfuatilie.
Maoneno hayo yalikuja baada ya kumuuliza swali juu ya alichokisema Kala Pina, kwamba Chid ameathiriwa na madawa, ndipo Chid alipojibu,“Sasa yeye mwenyewe mbona anavuta ganja, vitu kibao anafanya, sasa kwani mbona mimi simtangazii kwenye media, mimi sina habari, yeye kama ananifatilia hivyo nashukuru kumbe mimi ni bonge la star.
Aliendelea Chid akisema, “Umeona mwandishi watu wanahisi nimepotea, wakati kina Pina wananifatilia hadi maisha yangu, oohhh navuta nini…., sijui nimetoboa nini….., nilihisi hajawahi kuniona na kaona nimefanya nini…., nimevaa niko nini……, kumbe wananiona hivyo hadi nafanya nini, safi sana…” Alimalizia Chid Beenz…

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post