Unknown Unknown Author
Title: DC NACHINGWEA AZINDUA KAMPENI YA KATA KWA KATA UTOAJI WA ELIMU YA AFYA YA JAMII CHF
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mkuu wilaya ya Nachingwea,Regina Chonjo akifungua Mpango wa Uhamasishaji kata kwa kata wilayani Humo kwa wanachama na Wanufaika wa mfuko wa ...

clip_image001Mkuu wilaya ya Nachingwea,Regina Chonjo akifungua Mpango wa Uhamasishaji kata kwa kata wilayani Humo kwa wanachama na Wanufaika wa mfuko wa bima ya taifa ya afya na Wa Afya ya Jamii CHF kushoto ni Kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya,Aborgast Kiwale NHIF/CHF Mkoa wa Lindi na Fortunata Kullaya,Msimamizi w Mwenyekiti wa halmashauri ya Nachingwea, Abdalah Chikawe.clip_image002Msimamizi wa mfuko wa Taifa wa Bima Ya Afya wa mkoa wa Lindi ya afya,Bi Fortunata Raymond Kullaya akikabidhi barua Kwa Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea barua ya kukubaliwa maombi ya hospital ya Wilaya kukubaliwa kukopa Vifaa Tiba Kupitia Mfuko wa Bima ya Afya.clip_image002[13]Picha ya Juu na ya Chini: Baadhi ya Wanachama.clip_image002[15]

Na Abdulaziz Video,Nachingwea

Mkuu wa wilaya ya Nachingwea,Regina Chonjo ameitaka halmashauri ya wilaya hiyo kuhamasisha vituo vya kutolea tiba Pamoja na Hospital ya Wilaya kuomba mikopo ya vifaa tiba kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya ili kuboresha Utoaji wa Huduma za Tiba ikienda sambamba na Upatikananji wa Dawa.

Akifungua Mpango wa elimu kwa wanachama wa mfuko wa bima ya taifa ya afya na mfuko wa afya ya jamii,Mkuu wa wilaya hiyo alisisitiza kuwkutu kupitia maboresho ya mfuko katika Kuhudumia wanachama wake kunaendana na fursa za Upatikanaji wa huduma hivyo vituo vingi vinaweza kuboreka kihuduma ikiwa vifaa tiba vinakuwepo.

“Ningependa wilaya hii iwe kioo cha mafanikio ya utekelezaji wa sera ya mikopo ya vifaa tiba inayotolewa na mfuko huu na mkitumia fursa hizo tunaweza kuboresha huduma za matibabu kwa wanachama na jamii kwa Ujumla na Mkizingatia kuwa Mikopo ya NHIF inalipika kutokana na Huduma za wateja wao si vinginevyo;alimalizia uzinduzi huo na kuwapa fursa ya kutoa elimu hiyo kwa Kata zote 32 za wilaya hiyo.

Awali Bi Regina Chonjo Akizungumzia mpango huo wa elimu kwa wananchama na wadau wa mfuko huo,Aliitaka NHIF kwa kushirkiana na waajiri kuendelea na zoezi la kuwafikia wanachama hasa wale wanaoishi vijijini kwani unatoa fursa kwa wadau hao kutoa kero na kupokea maelekezo yenye ufafanuzi juu ya haki,wajibu za wanachama na maboresho ya kitita cha mafao.

‘Utaratibu wa kukutana na wanachama katika maeneo yao ya kazi ni utaratibu unaonyesha nia njema ya kuendeleza uwazi ,ushirikishwaji na uwajibikaji katika sekta ya afya na maendeleo ya mfuko Hivyo nashawishi asasi zote za umma kuwa na mfumo unaofanana na huu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kujali wateja wake”alisema Chonjo.

Kwa Upande wake Msimamizi wa Mfuko Huo Bi Fortunata Kullaya alieleza kuwa mpango huo ni moja ya mikakati ya mfuko huo kupata maoni ya wateja wao ikiwa pamoja na kutafuta namna ya kuboresha huduma ili kila mmoja apate Afya njema ambapo tayari mafunzo elekezi ya kata kwa kata katika mkoa wa Lindi yamefanyika katika wilaya za Liwale na Ruangwa

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top