AFANDE SELE AMTAJA MSANII YOUNG KILLER KAMA MSANII WA HIPHOP ANAYEMKUBALI ZAIDI. SOMA ZAIDI HAPA

clip_image001Unapozungumzia wasanii wapya wa hip hop Tanzania wanaonekana kuwa tishio kwa wasanii wengine hasa wakongwe si rahisi kuacha kuwataja wasanii kama Young killer na Stamina.
YAS2Kupitia XXL ya Clouds FM (May 23) rapper mkongwe Selemani Msindi a.k.a Afande Sele a.k.a King Selemani amethubutu kum’salute’ Young Killer kwa kusema ni msanii mkali ambaye anapaswa kuangaliwa sana hasa na wakongwe kutokana na ukali alionao katika hip hop.
Kwa kuonesha msisitizo kwa wasanii wakongwe wenzake amewashauri wasome sana vitabu kama njia ya kuweza kukabiliana na ushindani unaoletwa na wasanii wapya katika muziki wa kizazi kipya Tanzania ambao wameendelea kuwa tishio.
Young Killer anayetokea Rock City, alianza kung’ara kupitia shindano la Super Nyota lililoendeshwa na Clouds FM mwaka jana (2012) kwaajili ya kupata vipaji vipya vilivyoshiriki katika show kubwa ya Fiesta kwa mwaka huo. Stamina yeye anayetokea mji kasoro bahari Morogoro, ni msanii ambaye jina lake lilianza kukua taratibu kama unavyopanda ngazi.
Mpaka sasa amefanikiwa kuingia katika KTMA 2013 katika category 3 za, msanii bora wa hip hop, mtunzi bora wa mashairi ya hip hop na wimbo bora wa hip hop.
Kwa sasa Young Killer na Stamina wana collabo inayofanya vizuri katika vituo mbali mbali vya radio hapa bongo uliotoka siku za hivi karibuni, ‘Jana na Leo.’

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post