Lakini waliwatuliza na baadaye kufanya mchezo uwe wa mashambulizi kwa zamu kila upande. Dakika moja kabla ya mapumziko, Robin van Persie aliipatia Man United bao la kusawazisha baada ya yeye kuangushwa na Sagna katika eneo la 18.Kipindi cha pili kilikuwa cha mashambulizi ya zamu kila upande na mwisho Man United ambao tayari wamekuwa mabingwa wapya England wakatoka na sare hiyo ugenini.
Burudani nyingine uwanjani hapo ilikuwa ni kuonekana kwa rapa maarufu Jay Z wa Marekani ambaye alikuwa jukwaani akishuhudia mechi hiyo moja kwa moja.matokeo mengine, Chelsea ilifanikiwa kuinyoosha Swansea kwa mabao 2-0 na kuzidi kuweka uhai wa kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kufikisha pointi 65 ikiwa katika nafasi ya tatu, ikiwa na mchezo mmoja mkononi tofauti na Arsenal yenye pointi 64 katika nafasi ya nne.
Tags
SPORTS NEWS