Abdala Ulega Mkuu wa wilaya Kilwa akiwahutubia wazazi na wadau wa Elimu mjini Kilwa.
Serikali ya wilaya ya kilwa imewataka wazazi na walezi wanaokatakaza watoto wao kwenda shule wachukuliwe hatua za sheria ili kukomesha vitendo hivyo.
Agizo hilo limetolewa na mkuu wa wilaya Kilwa Abdala Ulega wakati
alipokuwa anazungumza na wazazi walezi na wadau wa elimu wa shule ya sekondari mibuyuni wilayani humo jana.
Ulega alisema kufanya hivyo sio tu kwamba ni kuwa nyanyasa bali pia
ni kuwanyima hakiyao ya msingi na urithi wa maisha yao ya baadaye
watoto ambao ndiyo tegemeo la taifa.
Watendaji wa tarafa, kata, kijiji wametakiwa kutekeleza agizo hilo
kwa kuwachukulia hatua wazazi na walezi aina hiyo.
Ulega alitoa agizo hilo baada ya kupata taarifa kuwa zaidi ya watoto
200 wa shule ya sekondari Mibuyuni hawafiki shuleni kutokana na utoro wa rejareja na kusababisha shule hiyo kuwa na mahudhurio madogo kila siku.
Aidha shule ya sekondari mibuyuni ambayo iko katika wilaya Kilwa
Mkoani Lindi ni kati ya shule 10 zilizofanya vibaya katika matokeo ya
kitado cha nne mwaka huu.
Tags
HABARI ZA KITAIFA