SEHEMU YA 12 YA TAMTHILIYA YA SIRI YA MTUNGI..!

Cheche anapata mkataba wa kufurahisha wa kupiga video ya muziki wa Bongo Flava. Ni kazi anayoifanya kwa mara ya kwanza. Lakini pale anapomsahau Shoti kwenye baa moja ya barabarani, Mwanaidi anaanza kupoteza uvumilivu wake kwa mkwewe mzembe.
Ni mwanzo mpya kwa Stephen katika shule nyingine. Duma anaanza kuelewa kwamba anawajibika kumtunza mdogo wake na hali kadhalika yeye mwenyewe.
Farida yumo kwenye njama ya kumfanyia ufidhuli Nusura na mimba yake. Lakini mapambano yake yanaposhindikana, anamwendea kinyume Kizito na kuelekea kwa Mgongo, mganga wa kienyeji, na kwa Furaha, fundi cherehani mmbeya.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post