BASTA AWAJIA JUU WAHUDUMU WA MGAHAWA

BASTA
Rapa mkongwe Basta Rhymes amepamba tena vichwa vya habari baada ya kuwawakia wahudumu wa mgahawa maarufu wa Cheeseburger Baby ambapo alikwenda kununua baga na kutakiwa kukaa katika foleni ili ahudumiwe kama watu wengine kitu ambacho hakukubaliana nacho kutokana na hadhi yake ya usupa staa.
Busta ambaye alifikia hadi hatua ya kutoa lugha chafu katika tukio hili alipandwa na hasira na kuamua kusubiria oda yake katika gari alilokuja nalo na hata baada ya kupatiwa alichoagiza alirudi tena katika mgahawa huu na kutukana wahudumu hali iliyosababisha wahusika kuita polisi kwa kuhofia usalama wao.
Kama hiyo haitoshi Basta ambaye aliondoka katika mgahawa huu kabla ya polisi kufika kwa hasira aliamua kuwapigia simu tena kudai kuwa oda yake aliyotoa haikuwa na kila kitu alichoagiza kitu ambacho wenye mgahawa wenyewe walikanusha na kusema sio kweli.
Kwa mujibu wa moja ya wafanyakazi wa mgahawa huu ambaye ametambulika kwa jina la Vitori, Mgahawa wao umekwishawahi kuhudumia watu maarufu kama vile rapa Jay Z na wengineo ambao waliweza kufuata utaratibu wao wa huduma kwa foleni bila shida.
Previous Post Next Post