Umoja wa Ulaya umezionya nchi wanachama wa Umoja huo kuweka mikakati imara dhidi ya biashara ya kuuza binaadamu isiokubalika au ziwekewe vikwazo.
Ripoti ya halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya, imesema tangu mwaka wa 2008 hadi mwaka wa 2010 biashara ya kuuza watu imeongezeka kwa asilimia 18 katika mataifa 27 yanayounda Umoja wa Ulaya.
Kulingana na kamishna anayeshughulika na maswala ya jamii katika Umoja huo Cecilia Malmstroem, Wanawake wanaume na watoto wanaendelea kuuzwa katika biashara ya ngono, kazi ngumu, ndoa za kulazimishwa, kazi za nyumbani, kuomba au hata kutolewa sehemu zao za mwili kwa ajili ya biashara. "Huu ni ukweli unaouma," alisema kamishna Malmstroem.
Kamishna wa Umoja wa Ulaya katika maswala ya Jamii Cecilia Malmstroem
Utafiti uliofanywa mwezi Juni mwaka jana na shirika la kazi duniani, ulikadiria takriban watu 880,000 walilazimika kufanya kazi ngumu katika mataifa ya Ulaya, jambo ambalo linatarajiwa kuongezeka kutokana na mgogoro wa uchumi, unaoshuhudiwa kwa sasa katika baadahi ya nchi, kwasababu raia katika nchi hizo hutafuta ajira za aina yoyote ile ili waweze kujikimu kimaisha.
Read more/Soma zaidi habari hii hapa »
Ripoti ya halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya, imesema tangu mwaka wa 2008 hadi mwaka wa 2010 biashara ya kuuza watu imeongezeka kwa asilimia 18 katika mataifa 27 yanayounda Umoja wa Ulaya.
Kulingana na kamishna anayeshughulika na maswala ya jamii katika Umoja huo Cecilia Malmstroem, Wanawake wanaume na watoto wanaendelea kuuzwa katika biashara ya ngono, kazi ngumu, ndoa za kulazimishwa, kazi za nyumbani, kuomba au hata kutolewa sehemu zao za mwili kwa ajili ya biashara. "Huu ni ukweli unaouma," alisema kamishna Malmstroem.Read more/Soma zaidi habari hii hapa »
Tags
HABARI KIMATAIFA