Na Mwandishi Wetu
KWA muda mrefu, zilisikika sauti za kupiga vita makundi ya wanawake yaliyosifika kwa kucheza utupu kwa kulowanisha khanga maji maarufu kama Khanga Moko Ndembendembe lakini sasa imeibuka nyingine, inayoitwa Fulana au Tisheti Ndembendembe, fahari ya kusini inabumburua.
Ilibainika kuwa staili hiyo ambayo ilianzia Pwani ya Kenya, sasa inatumiwa kudhalilisha warembo Uswahilini hasa kwenye ngoma maarufu za ‘kigodoro’ ambazo huchezwa bila kujali rika mbalimbali zinazokuwa zimechanganyikana.
Ilifahamika kuwa staili hiyo imewavutia wengi na vikundi vya uchezaji huo vimeanza kuundwa japo havijapata umaarufu mkubwa.
Mamlaka na wizara husika zinatakiwa kukemea kwa nguvu zote kwani huo ni mwanzo mwingine wa mmomonyoko wa maadili ya Kitanzania na ongezeko la maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU).
Tags
HABARI ZA KITAIFA