Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti Muzdalifa,Sheikh Abdalla Hadhal,alipoangalia maonesho ya picha mbali mbali wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto Yatima katika Ukumbi wa Salama Bwawani leo, maadhimisho hayo yamefanywa na Shirika la I.H.H la nchini Uturuki kwa ushirikiano na Jumuiya ya Muzidalifa ya hapa Zanzibar inayoshuhulika kna Mayatima.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea zawadi kutoka kwa Mtoto Hinaina Said Khalfan,wakati wa sherehe za siku ya Mtoto yatima zilizofanyika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel leo Mjini Zanzibar,shirika la misaada la I.H.H la Uturuki,kwa Ushirikiano na jumuiya ya Muzdalifa ya hapa Zanzibar kwa pamoja wamefanikisha kufanyika kwa sherehe hizo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akitoa hutuba yake wakati wa Sherehe ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto Yatima katika ukumbi wa Salama bwawani Mjini Zanzibar leo,maadhimisho hayo yamesimamiwa na jumuiya ya Muzidalifa na Shikika la misaada la I.H.H la Nchini Uturuki,(kushoto) makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif,Balozi wa Uturuki Nchini Ali Daudi Gul,na Waziri wa Katiba na Sheria,Abubakar Khamis Bakary,(kulia).BOFYA HAPA KWA HABARI NA PICHA ZAIDI
Tags
HABARI ZA KITAIFA