Kocha Athumani Kilambo akiwa na kikosi cha Pan Africa kilichonyakua ubingwa 1982
Habari zilizotufikia hivi punde zinasema mchezaji huyo wa zamani wa Yanga na kocha wa Pan Africa amefariki dunia usiku huu baada ya kusumbuliwa na saratani ya koo kwa takriban miaka miwili. Hivi majuzi alitolewa hospitali ya Ocean Road jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa kwa zaidi ya majuma mawili. Msiba uko nyumbani kwake Mwananyamala B Kwa Mama Zakaria
Source: ISSA MICHUZI
Tags
SPORTS NEWS