Gareth Barry akimfunga kipa wake katika kipigo cha 3-1 juzi
KOCHA Roberto Mancini amewataka wachezaji wake Manchester City kujitahidi zaidi, baada ya kuchapwa mabao 3-1 na Southampton. Ingawa hakuwataja majina, lakini, Mancini alisema ni wachezaji wawili tu waliojituma kwa kuonyesha juhudi za kutosha Jumamosi wakati City wakifungwa na timu ambayo ilikuwa Daraja la Pili misimu miwili iliyopita.
Mancini alisema wachezaji wake 15 walikuwa nje kwa majukumu ya kimataifa wiki iliyopita na kwamba klabu hiyo imefanya makosa katika dirisha dogo kutoimarisha kikosi kwa kusajili, huku akinyoosha kidole kila mahali, ispokuwa kwake.
‘Wakati unacheza mpira ni wewe ni mchezaji mkubwa, lazima utekeleze majukumu yako, wakati wote,’ alisema Mancini. ‘Si wakati wote ni makosa ya kocha. Wachezaji lazima wawajibike — Lazima wawe..... kama sivyo, hawawezi kuchezea timu kubwa.
Sasa Man City Wako nyuma kwa point 12 katika mzimamo wa ligi hiyo baada ya Jana Man Utd kuishinda Everton kwa goli 2-0 huku RVP kifunga goli lake la 19 na kuendelea kuwa kinara kwa upachikaji wa mabao katika ligi hiyo msimu huu.
Tags
SPORTS NEWS