Unknown Unknown Author
Title: UFAFANUZI KUHUSU MSAMAHA WA KODI KWA WATUMISHI WA UMMA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Watumishi wengi wa Serikali na Mashirika na taasisi za Umma wamekuwa wakiuliza mara kwa mara kuhusu msamaha wa kodi katika ununuzi wa magar...

Watumishi wengi wa Serikali na Mashirika na taasisi za Umma wamekuwa wakiuliza mara kwa mara kuhusu msamaha wa kodi katika ununuzi wa magari yao kwa ajili ya kuwasaidia usafiri wa kwenda kutekeleza majukumu yao ofisini na kuwasaidia nyumbani katika shughuli zao mbalimbali za kijamii. Yafuatayo ni maelezo ya utaratibu wa kupata msamaha wa kodi kwa magari yatakayoingizwa au kununuliwa hapa nchini na watumishi wa umma au Serikali.
Msamaha huu unatolewa kwa mujibu wa GN. Na. 520 na 522 za mwaka 1995
Mtumishi wa umma ambaye kwa mujibu wa sheria anafaidika na msamaha wa ushuru katika vyombo vya usafiri ni mwenye ngazi ya mshahara ya TGS D au zaidi kwa upande wa serikali au inayolingana na hiyo kwa upande wa Taasisi zingine za serikali na mashirika ya umma. Mtumishi wa umma ambaye anaendelea na masomo yake hapa nchini au nje ya nchi haruhusiwi kupewa msamaha wa ushuru hadi pale atakapomaliza masomo yake na akaendelea na utumishi wa umma.
Aina ya vyombo vya usafiri vinavyohusika na msamaha
(a) Magari
Magari madogo aina ya saloon, Magari aina ya pick – up yenye uwezo wa kubeba mzigo usiozidi uzito wa tani mbili, Magari mengine ambayo hayabebi zaidi ya abiria tisa.
(b) Pikipiki za aina zote.

Aina ya Ushuru unaosamehewa

  • Ushuru wa forodha (Import duty)

  • Ushuru wa bidhaa (Excise duty)
Aina ya kodi/ada zinazotakiwa kulipwa (Hakuna Msamaha)
  • Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)
  • Ada za usajili
  • Pia ushuru wa bidhaa maalumu kwa magari yenye umri wa miaka kumi au zaidi toka kutengenezwa
  • Gharama za bandari
Taratibu muhimu za kufuataKujaza fomu ya maombi (Nakala nne) ambayo ni lazima iambatane na:-
  • Uthibitisho wa mwajiri
  • Nakala ya kitambulisho cha kazi
  • Kumbukumbu za ununuzi au uingizaji wa chombo husika cha usafiri hapa
  • Picha nne (4) za “passport size “ kwenye fomu ya maombi.
Baada ya kupata fomu za maombi TRA inatakiwa kuzifanyia uhakiki na iwapo ni sahihi hupelekwa Hazina kwa kwa ajili ya kuandika hundi kwa kiasi cha ushuru uliosamehewa na kuwasilisha TRA
Baada ya TRA kupata hundi toka Hazina taratibu zingine zitaendelea za kuruhusu chombo cha usafiri kutolewa kwa mwenye nacho baada ya kulipa kodi zingine na ada kama vile Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na ada ya usajili wa gari.
TAHADHARI!Kwa wale ambao wanaagiza vyombo vya usafiri toka nje wanashauriwa
kufanya utaratibu wa kupata msamaha wa ushuru kabla ya chombo husika hakijafika hapa nchini.
Ni kosa kisheria kuuza chombo cha usafiri kwa mtu mwingine ambaye hastahili
msamaha bila kwanza kulipa Ushuru/kodi iliyokuwa imesamehewa. Pia ni kosa
kutumia kwa shughuli za biashara.
Epukana na matapeli wakati wote wa kushughulikia msamaha unashauriwa kutumia mawakala wa forodha wanaotambuliwa na TRA

Kwa maelezo zaidi wasiliana na :
Mkurugenzi,
Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi
SIMU 2119343
Barua pepe info@tra.go.tz

About Author

Advertisement

 
Top