Unknown Unknown Author
Title: Michezo ya makundi yakamilika–AFCON 2013
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Michuano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zinazoendelea nchini Afrika Kusini, inakamilika hatua ya makundi. Kesho(leo) timu za Ivo...
Michuano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zinazoendelea nchini Afrika Kusini, inakamilika hatua ya makundi.
Kesho(leo) timu za Ivory Coast, Togo, Tunisia na Algeria zinakamilisha mzunguko huo katika kundi D.
Ivory Coast ndiyo inayoongoza kundi hili kwa kuwa na pointi 6, ambapo tayari wamefuzu kucheza hatua ya robo fainali, huku Algeria isiyopata pointi yoyote ikiwa imeondolewa katika mashindano hayo. Kwa hiyo ni timu za Togo na Tunisia zenye pointi tatu kila moja ndiyo zinapigana kuungana na Ivory Coast kucheza hatua ya robo fainali.
Katika mpambano wa kundi hili la D, Ivory Coast na Algeria zinakamilisha ratiba kutoka na matokeo yao mpaka sasa, huku Togo inayokabiliana na Tunisia ndizo zenye kibarua kigumu huku kila timu ikitakiwa kushinda mechi hiyo.
Ivory Coast inajivunia nyota wake kama Didier Drogba, Yahya Toure, Gervinho, Salomon Kalou, Emmanuel Eboue na wengineo wengi wanaosakata kabumbu la kulipwa nje na wale wa ndani.

Kocha Sami Trabelsi, wa Tunisia, ambaye aliingia kwa kishindo mwaka 2011 kwa kutwaa ubingwa wa mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za nyumbani, katika mashindano yaliyofanyika nchini Sudan, amepanga malengo ya kufika robo fainali katika michuano hiyo.
"Hili halina ubishi kuwa tuko katika kundi gumu kuliko yote manne ya kwanza, lakini hatulalamiki kujikuta katika kundi hili," amesema kocha Trabelsi.

"Wachezaji wangu kwa kweli wanajibidiisha na ninaamini tutafika mbali- huenda hatua ya mwisho ya kuamua nani bingwa," amesema, akirejelea fainali za mwaka 1996, wakati Tunisia ilipofungwa na Afrika Kusini katika fainali mjini Johannesburg.

Kwa upande wa Togo itakuwa ikiwategemea nyota wake kadhaa akiwemo Emmanuel Adebayor.
Kwa hiyo ni mpambano mkali ambao utahusisha juhudi za wachezaji na makocha wa timu zote mbili.
Mpaka sasa kundi A zimefuzu timu za Afrika Kusini na Cape Verde, kundi B ni Ghana na Mali, C ni timu za Nigeria na Burkina Faso.











About Author

Advertisement

 
Top