Unknown Unknown Author
Title: YANGA WAFIKA SALAMA UTURUKI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Uwanja wa Ndege wa Istanbul ambako Yanga wapo kwa sasa YANGA SC, mabingwa mara tano wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Ka...
Uwanja wa Ndege wa Istanbul ambako Yanga wapo kwa sasa
YANGA SC, mabingwa mara tano wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame wamefika salama Istanbul, Uturuki kiasi cha saa moja iliyopita na sasa wanasubiri ndege ya kuunganisha kwenda Antalya, ambako wataweka kambi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Abdallah Ahmad Bin Kleb ameiambia LINDI YETU mida hii kwamba, amewasiliana na Mkuu wa Msafara, Mohamed Nyenge kampa taarifa hizo.
Yanga itaweka kambi katika mji wa Antalya uliopo kusini mwa Uturuki na itafikia katika hoteli ya Sueno Beach iliyopo pembezoni mwa bahari ya Meditreanian, na itakua ikifanya mazoezi katika viwanja vikubwa viwili vilivyopo katika hotel hiyo na kiwanja kidogo cha nyasi bandia.
Yanga iliondoka Dar es Salaam Alfajiri ya leo, saa 10:30 ikiwa na kikosi kamili; makipa; Ally Mustafa 'Barthez', Said Mohamed na Yussuf Abdul, mabeki Juma Abdul, Shadrack Nsajigwa, Godfrey Taita, Stefano Mwasyika, Oscar Joshua, Mbuyu Twite, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Ladisalus Mbogo na Kelvin Yondani.

Viungo ni Athumani Iddi ‘Chuji’, Frank Domayo, Haruna Niyonzima, Kabange Twite, Nurdin Bakari, Omega Seme, Simon Msuva, Rehani Kibingu, Nizar Khalfani na David Luhende wakati washambuliaji ni Didier Kavumbagu, Said Bahanunzi, Jerry Tegete, George Banda na Hamisi Kiiza.
Upande wa benchi la ufundi ni Kocha Mkuu Mholanzi, Ernie Brandts, Kocha Msaidizi Freddy Felix Minziro na Kocha wa makipa, Razak Ssiwa, na Maofisa wengine ni Daktari wa timu, Sufiani Juma, Meneja Hafidh Saleh, Ofisa Habari, Baraka Kizuguto Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Mohammed Nyenge.




About Author

Advertisement

 
Top