Unknown Unknown Author
Title: YANGA KUUMANA NA TUSKER YA KENYA (BOXING DAY) - TAIFA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Klabu ya Young Africans Sports Club itashuka dimbani siku ya jumatano (Boxing Day) kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Tusker FC ya nchin...
Klabu ya Young Africans Sports Club itashuka dimbani siku ya jumatano (Boxing Day) kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Tusker FC ya nchini Kenya, mchezo utakaofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Akiongea na waandishi wa habari Afisa Habari wa Yanga Baraka Kizuguto amesema Kocha wa Yanga anatarajiwa kuwatumia wachezaji wake wote katika mchezo huo ambapo Yanga itatumia nafasi hiyo kuwatumia karibu wachezaji wake wote ambapo timu hiyo inajiandaa kwa maandalizi ya safari ya kuelekea nchini Uturuki kwa maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara.
Mchezo huo utakua mchezo wa kwanza kwa Yanga tangu ligi iliposimama mwezi novemba baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa ligi Kuu ya Vodacom, hivyo itakua ni fursa kwa wanachama kuona timu yao ambayo ilianza mazoezi tangu tarehe 26 Novemba kujiandaa na mashindano mbali mbali aliesema "Kizuguto"

Pili itakua ni zawadi ya sikuuu ya X-Mass kwa wapenzi, wanachama na washabiki wa soka nchini, ambapo wapenda soka nchini watatumia fursa hiyo kusherekea sikukuu kwa kutazama soka safi ambalo hawajaliona kwa kipindi kirefu.
Tatu utakua ni mchezo wa mwisho katika kufunga mwaka kabla ya kusafiri kuelekea nchini Uturuki, pia ikitumia mchezo huo kuwaaga wapenzi, washabiki na wanachama wake kabla ya safari hiyo ya kambi ya mafunzo itakayochukua  ya takribani wiki 2.
Aidha Kizuguto ametangaza Viingilio vya mchezo huo kuwa ni Tsh 15,000/= VIP A, Tsh 10,000/= VIP B, Tshs 7,000/= VIP C, na Tsh 5,000/= kwa Orange, Blue na Green.
Kwa upande wa waandaji wa mchezo huo,  George Wakuganda amesema mchezo huo ni sehemu ya maandalizi ya Yanga na kwamba Yanga itatoa zawadi kwa mashabiki wake
Aidha amesema tayari wachezaji wa Tusker wameshawasili jijini Dar es Salaam, na kwamba mashabiki wa Yanga wajipange kupata burudani waliyo ikosa kwa kipindi kirefu kwa timu yao.
source: Young africa Web





About Author

Advertisement

 
Top