BREAK NEWS: MURJI KUTETA NA WAANDAMANAJI KESHO

1178[1]MBUNGE wa Mtwara mjini Hasnain Murji kesho saa Tisa alhasiri anatarajia kukutana na viongozi wa umoja wa vyama vya siasa vilivyoungana kupinga gesi kupelekwa Dar es Salaam.

Vingozi hao ndiyo walioratibu maandamano Alhamisi Desemba, 27 mwaka huu na kukusanya maelfu ya wananchi.

Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Mbunge huyo, Meckland  Millanzi tukio hilo litafanyika ukumbi wa kanisa la Pentekosite mjini Mtwara ambapo pia waandishi wa habari wamealikwa.

Millanzi hakuweza kuzungumzia ajenda za kikao hicho ila kwa mujibu wa Murji mwenyewe kikao hicho kitajadili  zaidi  namna  ambayo  wana Mtwara wanaweza kufaidika na gesi hiyo.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post