Unknown Unknown Author
Title: CCK KULIKONI?
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mwenyekiti wa CCK Constantine Akitanda (kushoto) na aliyekuwa Katibu Mkuu, Renatus Muabhi CHAMA cha Kijamii (CCK), kimeingia kwenye mgogoro...

Mwenyekiti wa CCK Constantine Akitanda (kushoto) na aliyekuwa Katibu Mkuu, Renatus Muabhi

CHAMA cha Kijamii (CCK), kimeingia kwenye mgogoro wa uongozi kutokana na viongozi wake wa juu kuhitilafiana baada ya Mwenyekiti Constantine Akitanda kumtimua Katibu Mkuu, Renatus Muabhi.
Tofauti za uongozi huo zilisababisha kuhitishwa mkutano wa Kamati Kuu na kuteuliwa Katibu Mkuu mpya, Kasimu Ismail Mtalam, uteuzi ambao Muabhi ameupinga.
Taarifa ya chama hicho kwa vyombo vya habari jana, ilisema kuwa mabadiliko hayo yalifanyika baada ya kamati kuu kukutana Juni 3, mwaka huu.
Chama hicho kimesema kuwa Muabhi na viongozi wengine wa zamani, akiwemo katibu wa wanawake, Dotto Njaa na Frida Mfuko aliyekuwa mweka hazina, watapangiwa kazi nyingine na chama.
Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana, Muabhi alisema kuwa mabadiliko hayo yamefanywa na Mwenyekiti Akitanda kwa kupanga safu yake.
Alisema kuwa vita ambayo walikuwa hawaelewani na Akitanda ni pamoja na kuwatafuta watu wengine kujiunga katika chama pasipo kuwepo na utaratibu kwa mujibu wa msajili wa vyama.
Muabhi alisema mkutano huo uliowaengua ulikuwa batili kwa kuweka mazingira ya kupeana madaraka bila ushirikishwaji wa viongozi wengine.

CHANZO: SAID POWA BLOG

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top