Unknown Unknown Author
Title: Vibaka wamliza Wema Sepetu
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Wema Isaac Sepetu, hivi karibuni alijikuta akipata wakati mgumu baada ya kukombwa vioo vya gari lake aina ya Toyota Mark X  na vibaka wa Mo...
Wema Isaac Sepetu, hivi karibuni alijikuta akipata wakati mgumu baada ya kukombwa vioo vya gari lake aina ya Toyota Mark X  na vibaka wa Moshi, Kilimanjaro.
Tukio hilo limetokea hivi karibuni ndani ya Viwanja vya Chuo cha Ushirika  ambapo staa huyo alikuwa amehudhuria uzinduzi wa Tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Akiwa katika burudani hizo, Wema  ambaye muda mwingi alionekana kuwa mtu mwenye furaha ghafla alibadilika na kuishiwa na furaha alipolikuta gari lake likiwa limekongolewa vioo vyote vya pembeni.Tulizungumza na  Wema  kuhusu tukio hilo ambaye alionekana  kushangazwa  na tukio hilo na kusema kuwa  hakutarajia  kukutana nalo  kwa kuwa alikuwa  akiwaheshimu sana watu wa Moshi.
“Imeniuma sana baada ya kukuta gari langu limekongolewa,  wameiba vioo na ukiangalia nipo ugenini, halafu magari ni mengi yaliyokuwa yamepaki uwanjani, kwa nini yasiibiwe hayo mengine wakaiba langu tu, dah! imenikera sana,” alisema Wema kwa uchungu.
Hilo ni tukio lingine la Wema kulizwa, alishawahi kuibiwa nyumbani Sinza jijini Dar baada ya wezi kuruka ukuta na kumkomba baadhi ya vitu vya thamani, pia alishawahi kuibiwa vitu vingine ndani ya gari Uwanja wa Taifa.

About Author

Advertisement

 
Top