Rais Jakaya Kikwete Amwapisha Mtendaji Mkuu wa Mahakama pamoja na Msajili Mkuu wa Mahakama na Msajili wa Mahakama ya Rufani

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amemwapisha Mtendaji mkuu wa Mahakama pamoja na Msajili mkuu wa Mahakama na msajili wa mahakama ya rufani katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam.Walioapishwa leo ni Mtendaji mkuu wa Mahakama Bwana Hussein Katanga,Msajili Mkuu wa Mahakama Bwana Ignus Paul Kitusi na Msajili wa Mahakama ya Rufani Bwana Panterine Muliisa Kente.Pichani Mtendaji mkuu wa Mahakama Bwana Hussein Katanga akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue(kushoto) pamoja na maofa waandamizi wa mahakama aliowaapisha leo asubuhi ikulu jijini Dar es Salaam.(Wapili kushoto) ni Mtendaji mkuu wa Mahakama  Bwana Hussein Katanga,(Wanne kushoto) ni Msajili Mkuu wa Mahakama Bwana Ignus Paul Kitusi na kulia ni Msajili wa Mahakama ya Rufani Bwana Panterine Muliisa Kente.Picha na Freddy Maro-IKULU

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post