Unknown Unknown Author
Title: GADNA G HABASH ATUA RASMI RADIO TIMES FM
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
MTANGAZAJI Super Star bongo, Gadna G. Habash leo ametambulishwa rasmi kuhamia Radio Times FM, baada ya kuwa nje ya kazi kwa takriban miaka ...
MTANGAZAJI Super Star bongo, Gadna G. Habash leo ametambulishwa rasmi kuhamia Radio Times FM, baada ya kuwa nje ya kazi kwa takriban miaka miwili, tangu aipige chini Clouds FM.
Sauti tamu ya mume huyo wa mwanamuziki nyota Tanzania, Lady Jaydee sasa itakuwa ikisikika kwenye kipindi cha Maskani, kuanzia saa 10:00 jioni hadi saa1:00 usiku.
Gadna kushoto akiwa na Schola na mtangazaji mwingoine mpya wa Times, Natasha ambaye anatangaza kipindi cha Filamonata.
Mara ya mwisho, Kapteni G alikuwa akitangaza kipindi cha Jahazi Clouds kabla ya kubwaga manyanga Novemba mwaka 2010 katika kipindi ambacho redio hiyo ilipoteza mastaa wengi, wakiwemo Fina Mango, George Njogopa na Masoud Kipanya.  
Fina kwa sasa yupo Magic FM na Kipanya alimtangulia Gadna Times.William Malacela akimpongeza GadnaWaandishi wa Habari waliohudhuria utambulisho wa Gadna Times FM leo wakipata maakuli


About Author

Advertisement

 
Top