Rooney ni nyota ya England

Wayne RooneyWayne Rooney alikaribishwa kama shujaa katika timu ya England usiku wa Jumanne, baada ya kutokuwepo kwa muda kufuatia adhabu ya UEFA, na bao lake moja dhidi ya Ukraine liliiwezesha timu yake kuwa kileleni katika kundi la D.

Vile vile bao hilo linamaanisha England imeweza kuiepuka Uhispania katika robo fainali, na sasa itacheza dhidi ya Italia.

Rooney, akiwa karibu sana na kipa wa Ukraine, Andriy Pyatov, aliweza kufunga kwa kichwa, mpira uliokuja juujuu kutoka kwa nahodha Steven Gerrard.

Licha ya England kuibuka washindi, Ukraine walifanya juhudi kubwa na kupata nafasi nyingi zaidi za kusawazisha, lakini yote hayo hayakufua dafu.

Ukraine walistahili kupata bao wakati mkwaju wa Marko Devic ilikuwa wazi umevuka mstari, lakini kufuatia juhudi za John Terry katika kuondosha mpira huo, pengine mwamuzi alishawishika kwamba kweli mpira haukuvuka msitari.

Ushindi wa Sweden wa magoli 2-0 dhidi ya Ufaransa ulihakikisha kwamba England wanafuzu kuingia robo fainali kama timu iliyoongoza katika kundi D.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post